IQNA

Mashindano ya 19 ya Kimataifa ya Qur’ani Kuwait yaanza

17:45 - September 01, 2015
Habari ID: 3356079
Mashindano ya 19 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Kuwait yameanza Jumatatu hii.

Idara kuu ya Awqaf nchini Kuwait imesema mashindano hayo yanalenga kuanzisha thamani za Kiislamu katika jamii, kuhimiza watu kuhifadhi na kuisoma Qur’ani Tukufu na kuwaunga mkono wale wanaochangia kufikia malengo hayo.
Naibu Katibu Mkuu wa Idara Kuu ya Awqaf Kuwait na mkuu wa kamati andalizi ya mashindano hayo Mohammad Al-Jahama amesema kumekuwepo na ushajiishaji katika vyombo vya habari ili kuwahimiza Wakuwait kushiriki katika mashindano ya Qur’ani.
Ameongeza kuwa zawadi za mashindano hayo ni Dirhamu za Kuwait (KD) 6,000 kwa mwenye kuchukua nafasi ya kwanza, 5,000 kwa nafasi ya pili, 4,000 kwa atayakepata nafasi ya tatu na 3,000 kwa atakayechukua nafasi ya nne.../mh

3355790

captcha