IQNA

Misri kuandaa mashindano mawili ya Qur’ani

10:28 - March 12, 2015
Habari ID: 2968365
Misri itakuwa mwenyeji wa mashindano mawili ya kimataifa ya Qur’ani katika miezi michache ijayo.

Mashindano ya kwanza yamepangwa kufanyika Aprili 18-23 na yameandaliwa na Wizara ya Awqaf Misri. Wawakilishi wa nchi 50 wanatazamiwa kushiriki katika mashindano hayo yaliyopewa anuani ya:  “Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu na Ufahamu wa Maadili Yake”.
Tayari nchi 15 ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia, Burundi na Uingereza zimeshatangaza kuwa tayari kutuma wawakilishi wao.
Mashindano ya pili ya Qur’ani yanatazamiwa kufanyika mwezi Juni chini ya usimamizi wa Kituo cha Kiislamu cha Chuo Kikuu cha Al Azhar.
Mashindano hayo yaliyopewa anuani ya ‘Mashindano ya Kimataifa Kuhusu Ijaz Qur’ani na Sunnah an-Nabawiyyah ‘ yatajumuisha makala za utafiti kuhusu  miujiza ya Qur’ani na Seerah ya Mtume SAW.../mh

2957672

captcha