IQNA

Harakati za Qur'ani Tukufu

Mkuu wa Al-Azhar awaenzi washindi wa mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu

12:57 - June 03, 2023
Habari ID: 3477087
TEHRAN (IQNA)- Sheikhe Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri amewatunuku washindi wa Mashindano ya Kila Mwaka ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu ya Al-Azhar.

Sheikh Ahmad al-Tayyeb alitoa  shukrani za dhati za Al-Azhar kwa wanafunzi wake waliohifadhi Qur'ani, na akawatangaza kuwa mabalozi bora wa kituo hicho cha Kiislamu.

Aliamua kuongeza mara mbili ya zawadi kwa washindani watano bora wa kategoria ya 1, na hivyo tuzo ya mshindi wa kwanza ya kitengo cha 1 inakuwa 200,000 EGP. Jumla ya washiriki walioongezwa hadi wanafunzi 180,000, kati yao 59,000 walifaulu mtihani wa awali. Kisha, wanafunzi 18,000 walifaulu mtihani wa hatua ya pili, huku 1,202 wakipitia awamu ya mwisho ya kuchagua kumi bora nchini kote.

Katika awamu ya awali, Esra El-Sayed Saad Muhammed alikuja wa kwanza, ‎na kushinda zawadi ya EGP 200,000; huku Ziyad Muhammed ‎Mustafa akishika nafasi ya pili, akishinda zawadi ya EGP 190,000. Kisha, ‎Ahmed Gamal Es-Sayed Hashish alishinda nafasi ya tatu, akipokea zawadi ya EGP 180,00, huku Iman Wael Ahmed Gharib, akishika nafasi ya nne, akipokea zawadi ya EGP 170,000, na mshindi wa tano alikuwa Malak Walid Kamel Ibrahim, kupata zawadi ya ‎160,000 EGP.‎

Wakuu wa Al Azhar wanasema mashindano hayo yanalenga kuhimiza uhifadhi na masomo ya Qur'ani miongoni mwa vijana, kubaini vipaji vya ubunifu miongoni mwao, na kuwatayarisha kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu.

3483805

Kishikizo: qurani tukufu azhar
captcha