IQNA

Zaka ni Wajibu Katika Dini kwa Waislamu Kabla ya Uislamu

14:12 - October 12, 2023
Habari ID: 3477720
TEHRAN (IQNA) - Zaka ni wajibu wa kidini kwa Waislamu ambao wanakidhi vigezo muhimu vya kuchangia sehemu fulani ya baadhi ya mali zao.

Zaka haishii tu kwa Uislamu tu bali ilikuwepo katika dini za awali pia, Kwa hakika, Zaka na maombi ni mambo ya kawaida katika imani zote za Mwenyezi Mungu.

Nabii Isa (A.S) alianza kuzungumza katika utoto wake, akisema, Mwenyezi Mungu alinijaalia sala na Zaka kwa muda wote nitakaoishi tafsiri ya  aya ya 31 ya Sura Maryam.

Nabii Musa (A.S) aliwaambia Bani Israil; Simamisheni Sala zenu, toeni Zaka, na rukuuni na sujuduni pamoja na wanaorukuu, tafsiri ya  aya ya 43 ya Sura Al-Baqarah.

Qur’ani Tukufu  inasema kuhusu Nabii Ismail (AS) Na akawaamrisha watu wake kuswali na kutoa sadaka kwa  Mola wao Mlezi akaridhika naye,tafsiri ya  aya ya 55 ya Sura Maryam.

Qur’ani Tukufu pia inasema kuhusu Mitume wa Mwenyezi Mungu kwa ujumla; Sisi tumewaweka viongozi wa kuongoza kwa amri yetu na tukawafunulia kutenda mema, na kusimamisha Sala, na kutoa Zaka, na walikuwa kwa ajili yetu waakiomba na kumcha Mola wao Mlezi, aya ya 73 ya Sura Al-Anbiya.

Falsafa ya Khomsi na Zaka katika Uislamu

Pia, kwa mujibu wa aya ya 5 ya Sura Al-Bayyinah Mwenyezi Mungu anasema, Hawakuwa wameamrishwa tu kumwabudu Mwenyezi Mungu, na wasimamie dini yake, wasimame katika Sala, na watoe Zaka hakika hii ndiyo dini ya milele na daima Kwa hivyo katika dini zote za Mwenyezi Mungu Zaka imeambatana na sala.

Msomi Allameh Tabatabaei anasema kuhusu Zaka kwamba ingawa kanuni za kijamii zilizoletwa na Uislamu ni kamilifu zaidi kuliko zile za dini zilizopita, sio uvumbuzi wa Uislamu, bali zilikuwepo kabla. Inaweza kusemwa kwamba hakukuwa na watu katika historia ambao hawajafuta sheria za kifedha za kuendesha jamii kwa sababu kila jamii inahitaji njia za kifedha kufanya kazi na kukua.

 

3485524

captcha