IQNA

Zakzaky akiwa Tehran: Alikaribishwa kwa Furaha na Umati mkubwa wa Watu Mjini Tehran

9:57 - October 12, 2023
Habari ID: 3477718
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) Sheikh Ibrahim Zakzaky alikaribishwa kwa furaha na umati mkubwa wa watu mjini Tehran.

Sheikh Zakzaky na mkewe waliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeini Jumatano asubuhi.

Ameandamana na mkewe, Malama Zeenah Ibrahim, wako nchini Iran kwa matibabu, kulingana na Mkuu wa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kiislamu yenye makao yake London (IHRC) Massoud Shajareh.

Mamia ya watu, wengi wao wakiwa wanafunzi, walikuwa wamekusanyika katika uwanja wa ndege tangu asubuhi kumkaribisha Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN),  Walibeba mabango ya kuunga mkono Zakzaky, Mapinduzi ya Kiislamu  ya Iran na upinzani.

Alihutubia kwa ufupi umati wa watu alipowasili na kusema;Mwenyezi Mungu akipenda,  Mapinduzi ya Kiislamu yataleta mabadiliko kote duniani ikiwemo Marekani na Ulaya, ili kuandaa mazingira ya kurejea Imam wa mwisho wa Mashia, Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake).

Nina furaha sana kwamba watu kama hao wanaunga mkono upinzani na sina maneno mengine ya kusema isipokuwa kukushukuru, alisisitiza;

Kwa mujibu wa Shajareh, ambaye kwa miaka mingi alitaka kuhakikisha wanaachiliwa huru wawili hao na matibabu kwa ajili yao, alibainisha kuwa Sheikh Zakzaky alipoteza jicho lake wakati vikosi vya jeshi la Nigeria vilipovamia nyumba yake miaka iliyopita.

Alisema makumi ya risasi zimesalia mwilini mwake na pia kuna dalili za sumu ya risasi kwenye damu yake.

Mkewe, Malama Zeenah Ibrahim , pia ana maumivu makali ya goti na hawezi kutembea, aliongezakwa kusema,

Kwa vile hali hazikuwa nzuri kwa ajili ya kuendelea na matibabu yao nchini Nigeria, uwanja uliandaliwa kwa ajili ya safari yao ya kwenda Iran kwa matibabu, Shajareh alibainisha.

Alisema mipango kadhaa zimepangwa kufanywa wakati wa kukaa kwao nchini Iran na Sheikh Zakzaky pia amepangwa kupokea PhD ya heshima katika Chuo Kikuu cha Tehran.

Sheikh Ibrahim Zakzaky ni nani?

Mwezi Desemba  mwaka 2015, jeshi la Nigeria lilianzisha msako mkali kama sehemu ya upanuzi mbaya ulioamriwa na serikali kulenga vuguvugu ambalo Abuja imelitaja kuwa haramu.

Kampeni hiyo ilishuhudia wanajeshi wakishambulia makazi ya sheikh Zakzaky katika mji wa Zaria huko Kaduna, na kumsababishia majeraha mabaya yeye na mkewe ambayo yaliripotiwa kusababisha Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria huyo kupoteza jicho lake la kushoto.

Serikali ya Nigeria Inaendelea Ukiukaji wa Haki za Sheikh Zakzaky.

Wakati wa msako huo, wanajeshi pia waliwashambulia wanachama wa vuguvugu hilo walipokuwa wakifanya maandamano ya kidini, huku serikali ikidai kuwa Waislamu walikuwa wamezuia msafara wa waziri wa ulinzi wa nchi hiyo.

Vuguvugu hilo limekanusha madai hayo na kusema msafara huo ulivuka njia kimakusudi na wanachama  wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) ili kutoa kisingizio cha kuwashambulia.

Vurugu hizo zilisababisha vifo vya wana watoto watatu wa sheikh Zakzaky na zaidi ya wafuasi wake 300.

Malama Zeenah Ibrahim na sheikh Zakzaky  waliwekwa rumande kwa miaka mingi licha ya uamuzi wa mwaka wa 2016 wa mahakama kuu ya shirikisho ya Nigeria iliyoamuru waachiliwe kutoka gerezani.

Shiekh Zakzaky Atoa Wito wa Kususia Kiuchumi dhidi ya Mataifa ya Nordic kuhusu Kuvunjiwa heshima Qur’ani Tukufu.

Katikati ya kifungo cha muda mrefu gerezani, waliruhusiwa kuondoka kwenda India kwa madhumuni ya matibabu, hata hivyo, kuliripotiwa kukumbwa na kuingiliwa na serikali kwa lengo la kuwazuia kupata matibabu sahihi.

Uhuru wa Malama Zeenah Ibrahim na sheikh Zakzaky,  ulikuja mwezi Julai mwaka 2021 kufuatia wanaharakati wasiochoka kwa upande wa waumini wa Shia wa Nigeria na ripoti za mara kwa mara kuhusu hali zao na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu.

 

 

 

3485536

 

 

 

 

captcha