Ee Mwenyezi Mungu! Niongoze katika mwezi huu kwenye amali njema, Unitekelezee katika mwezi huu haja zangu na mataraji yangu, Ewe Usiyehitaji ufasiri na kuuliza (ndipo ukaifahamu haja ya mja, bali Unaifahamu hata bila ya kuuliza na bila kuelezwa). Ewe Mjuzi wa yalioyomo vifuani (nyoyoni) mwa walimwengu! Mteremshie rehema na amani (Mtume) Mohammad (s.a.w.) na Aali zake watakatifu.