Ee Mola wangu! nijaalie katika mwezi huu nilipate fungu la rehema zako pana, Uniongoze katika mwezi huu kwenye mwanga wako unaong'ara, na Uniongoze moja kwa moja kwenye radhi yako yenye kukusanya mahaba yako (yaani mambo yote Unayoyapenda na kuyaridhia) Ewe Karim.