IQNA

Qiraa ya Qur'ani Tukufu

Qari wa Misri apata mapokezi mema huko Bangladesh

18:29 - March 06, 2023
Habari ID: 3476667
TEHRAN (IQNA) – Maelfu ya watu walihudhuria mahafali ya kusoma Qur’ani Tukufu iliyofanyika Bangladesh ambapo qari wa Misri Mahmoud Kamal al-Najjar alisoma aya za Kitabu kitakatifu.

Hafla hiyo ilifanyika huko Gazipur, wilaya katikati mwa Bangladesh na sehemu ya mji mkuu, Dhaka na ilikuwa Mahafali ya 22 ua Qur’ani Tukufu ambayo huandaliwa kila mwaka wa Jumuiya ya Iqra ya Bangladesh.

Watu wa wilaya hiyo walimpokea kwa furaha msomaji huyo wa Qur'ani kutoka Misri.

Al-Najjar alisema alishangazwa kuona watu wengi katika mahafali hiyo ya Qur'ani Tukufu.

Alisema amesafiri katika nchi nyingi za Kiislamu na Kiarabu lakini hii ni mara yake ya kwanza kuona mapokezi hayo mazuri ya programu ya usomaji wa Qur'ani.

Al-Najjar, ambaye anatoka katika jimbo la Dakahlia nchini Misri, ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar.

Amesafiri katika nchi mbalimbali kama Kuwait, Pakistan, Uturuki, na India kwa ajili ya kushiriki katika vikao vya kusoma Qur'ani Tukufu.

Egyptian Qari Given Warm Reception in Bangladesh  

Egyptian Qari Given Warm Reception in Bangladesh  

Egyptian Qari Given Warm Reception in Bangladesh  

Quranic program in Bangladesh

4126330

captcha