Sheikh Naim Qassem ameandika kuwa: "Hongera kwa ushindi wa timu ya taifa ya Morocco na kufuzu kucheza robo fainali katika Kombe la Dunia, Qatar 2022. Mumeshinda mara mbili: Kwanza, kwa kufuzu kuingia robo fainali, na pili kwa kuinua juu bendera ya Palestina."
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwaambia wachezaji wa timu ya soka ya Morocco kwamba: Tunawapenda enyi simba, na tunaipongeza Palestina kwa kuwa na watu kama nyinyi.
Jana timu ya taifa ya Morocco iliishinda Uhispania kwa mabao matatu kwa bila katika mikwaju ya penalti katika mchujo wa kuwania kuingia robo fainali ya Kombe la Dunia, Qatar 2022. Ushindi huo unaifanya Morocco kuwa timu ya kwanza ya Kiarabu ya kaskazini mwa Afrika kufuzu kuingia raundi ya robo fainali katika historia ya Kombe la Dunia.
Wachezaji wa timu ya Morocco walisherehekea ushindi huo kwa kupeperusha bendera ya taifa linalokandamizwa la Palestina ambalo linakoloniwa na utawala haramu wa Israel. Kwa kupeperusha bendera hiyo, wachezaji wa Palestina walitangaza uungaji mkono wao kwa mapambano ya ukombozi wa Palestina na kibla cha kwanza cha Waislamu. Vilevile walionekana wakisuduju uwanjani wakimshukuru Mwenyezi Mungu kwa mafanikio hayo.
4105385