IQNA

Nchi za Waislamu zishirikiane kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu

21:40 - July 22, 2022
Habari ID: 3475524
TEHRAN (IQNA) - Mwanadiplomasia wa Iran amesisitiza ulizamia wa kuwepo ushirikiano wa karibu kati ya nchi za Waislamu kukabiliana na matukio ya chuki dhidi ya Uislamu au Islamophobia na kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu duniani.

Balozi wa Iran huko Pakistan Seyyed Mohammed Ali Hosseini amebainisha maoni hayo wakati wa mkutano na Waziri wa Shirikisho wa Haki za Binadamu Pakistan Mian Riaz Hussain Pirzada siku Alhamisi.

"Jukumu la Pakistan katika kufanikiwa kukabiliana na hatari ya Islamphobia ulimwenguni kwa njia za kidiplomasia ni ya kusifiwa."

Katika kikao hicho, Balozi wa Iran alimpongeza waziri Pirzada kwa kuteuliwa nafasi hiyo na kumtakia mafanikio katika kazi zake mbali mbali. Alisema kuwa Iran iko tayari kuimarisha ushirikiano na Pakistan katika  uwanja wa haki za binadamu na haswa ushirikiano wa mahakama.

Katibu wa haki za binadamu Afzal Latif na maafisa wengine waandamizi wa wizara pia walikuwepo katika mkutano huo. Wakati wa mkutano, pande zote mbili zilibaini azma ya kuongeza ushirikiano wa nchi mbili katika uwanja wa haki za binadamu.

Pirzada alisema Pakistan na Iran zina uhusiano wa kindugu wa zaidi ya miongo saba ambao uko kwa msingi wa utamaduni, dini na kihistoria.

Balozi wa Iran alisema serikali ya Iran inalipa uzito mkubwa na maalumu haki za wanawake na uwezeshaji wao.

Waziri wa Haki za Binadamu alisema kuna fursa kubwa ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili jirani. Alisema juu ya Pakistan inaipongeza Iran kutokana na ukarimu wake kwa wafanyaziara za kidini hasa kupitia mpaka wa Taptan.

"Tunapata msukumo wa haki za binadamu kutoka kwa mafunzo ya Nabii wetu Mtakatifu Muhammad SAW. Lakini sasa ulimwengu unatawaliwa na wale wanaodai kutetea haki za binadamu  lakini wenyewe ni wakiukaji wakubwa wa haki za binadamu. Aidha ameipongeza Iran kwa mapambano yake mbele ya propaganda na vikwazo vya kiuchumi ambavyo imewekewa na madola ya Magharibi hasa Marekani.

3479788

captcha