IQNA

Zaidi ya milo Milioni 3 ya futari yasambazwa katika Msikiti Mkuu wa Makka

17:32 - April 24, 2022
Habari ID: 3475164
TEHRAN (IQNA) - Zaidi ya milo milioni 3 ya futari ilitolewa kwenye Msikiti Mkuu wa Makka katika siku 20 za mwanzo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu wa 1423 Hijria Qamaria.

Vyombo vya habari vya Saudia vimeripoti kuwa, milo hiyo ilitolewa na mashirika ya misaada kwa kushirikiana na kamati ya serikali huko Maka.

Mamia ya wafanyikazi, wakiwemo 100 kutoka Idara Kuu ya Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu, wanasimamia usambazaji wa milo takribani 150,000 kwa siku, mkuu wa usimamizi wa uwanja wa msikiti huo Moussa bin Mohammed alisema.

Takriban mashirika 67 ya misaada yanajishughulisha na kutoa chakula hicho, na maeneo ya futari katika msikiti huo yameainishwa kwa uratibu na vyombo vya usalama, afisa huyo alisema.

3478621

captcha