IQNA

Usiku wa Laylatul Qadr; Fursa yenye upana wa maisha

18:04 - April 23, 2022
Habari ID: 3475158
“ Laylatul Qadri (Usiku wa Cheo Kitukufu) ni bora kuliko miezi elfu”. Hii aya ya 3 ya Surat Al-Qadr katika Qur'ani Tukufu.

Ramadhani ni mwezi wa sikukuu ya Mungu na moyo wa mwezi huu ni Laylatul Qadri (Usiku wa Cheo Kitukufu).

Ni usiku wa rehema ya Mwenyezi Mungu na msamaha wa dhambi na ni usiku mkubwa ambao unapendekezwa kuimarisha uhusiano na Mwenyezi Mungu kwa kusoma Qur'ani na kutekeleza Sala na dua kwa Mwenyezi Mungu.

Nasaha muhimu zaidi juu ya Laylatul Qadri ni kuamka au kukeshahadi kuchomoza kwa jua.

Katika kumi la tatu la Ramadhani, Mtume Muhammad SAW alikuwa akikusanya kitanda chake na kwenda msikitini kwa ajili ya itikafu, na ingawa msikiti wa Madina haukuwa na paa, alikuwa hatoki msikitini hata mvua inaponyesha. Alikuwa macho usiku kucha.

Wanazuoni wa Kiislamu  wamesema ukubwa na aina ya matukio ya mwaka huamuliwa katika usiku huu, yaani, Mwenyezi Mungu huamua mambo kama vile uhai, kifo, riziki, furaha na masaibu ya wanadamu (Tafsir al-Mizan) na hivyo matendo ya mwanadamu yanahusika katika katika hatima hii.

Masuala ya kimaanawi na maana ya hatima ya mambo ya ulimwengu yameelezwa katika vitabu vya Kiislamu. Lakini yanayopendekezwa kwenye usiku wa Laylatul Qadri (Usiku wa Cheo Kitukufu) yanalenga kuweka kumbukumbu ya Mungu hai nyoyoni. Kudhihirisha toba na kuomba msamaha wa dhambi na kuainishwa hatima ya siku zijazo ni mada zinazopatikana katika ibada za usiku hii. Hivi ndivyo ilivyo hasa katika dua maarufu za Abu Hamza al-Thumali  na Iftitah.

Ikiwa tunataka kuzingatia jina la usiku huu, lazima tuseme kwamba usiku wa hatima ni usiku wa mwanadamu kuekelea kwa  Mwenyezi Mungu. Mtukufu Mtume SAW amesema: Hakika matendo yote huzingatiwa nia.

Usiku wa Laylatul Qadri unalenga pia kuwa na taathira katika nia za mwanadamu.

Mengi ya matendo ya Waislamu yanafanana na ya wanadamu wengine, lakini katika sheria ya Kiislamu, kuna malipo yake. Kula, kunywa, kufanya kazi, kusoma sayansi, kusaidia masikini, nk, na hata waumini wanaolala na kupumua wakati wa Ramadhani wanalipwa. Kwa nini? Kwa sababu kila kitu kinafnayika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa nia ya kumkaribia Mungu na kupata sifa za kimaanawi. Utakaso wa nia ya mwanadamu unahitaji uamuzi mkubwa ambao unakuwa rahisi katika usiku wa Laylatul Qadri .

Ni kwa mtazamo huu ndio tunaitazama aya tuliyotangulia kuitaja isemayo: “Laylatul Qadri (Usiku wa Cheo Kitukufu) ni bora kuliko miezi elfu

Miezi elfu moja ni kama miaka 83, ambayo labda ni wastani wa maisha ya mwanadamu. Hivyo kimsingi ni kuwa katika usiku mmoja, mtu anaweza kufikia mafanikio ambayo kwa kawaida anapaswa kuyafikia katika umri wake wote. Mafanikio haya yanatokana na  nia safi wakati ambapo wakati mja anaposamehewa dhambi, tabia yake nayo pia hubadilika na huwa miongoni mwa wanadamu wema

Hatima ina maana ya kuamua ukubwa na matukio ambayo yameshaamuliwa na Mungu kwa ajili ya ulimwengu. Hatima haina ukinzani na uhuru wa hiari ya mwanadamu na suala la mamlaka, kwa sababu majaaliwa ya Mwenyezi Mungu ni kwa mujibu wa sifa za watu binafsi na kiwango cha imani na uchamungu na usafi wa nia na matendo yao. Hiyo ina maana kuwa, hatima imeamuliwa kwa

captcha