Kwa mujibu wa taarifa, Spika wa Bunge la Iran Mohammad Baqer Qalibaf aliwasili Uturuki Jumatano na kulakiwa na Osman Nuri Gülaçar,Mwenyekiti wa Kundi la Kirafiki la Mabunge ya Iran na Uturuki.
Akizungumza katika mapokezi hayo, Nuri amesisitiza kuhusu nafasi muhimu ya Iran katika eneo na kusema: "Inatazamiwa kuwa nchi hizi mbili zitachukua hatua za kuboresha uhusiano zaidi hadi ifikapo mwaka 2023."
Aidha amesema mabunge ya nchi hizi mbili yanaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuboresha uhusiano.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Iran ameashiria uhusiano wa mabunge ya Iran na Uturuki na kusema uhusiano wa nchi mbili uko katika kiwango kizuri na cha kurihdhisha na inatazamiwa kuwa uhusiano huo tazidi kuboreka.
Mkutano wa 16 wa Jumuiya ya Mabunge ya Kiislamu ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu unafanyika Istanbul Uturuki kuanzia Disemba 9-10 na mada kuu ni "Palestina, Uhamiaji na AfghanIstan.