Kwa mujibu wa amri iliyotolewa na Abdul Latif Al Sheikh, Waziri wa Masuala ya Kiislamu Saudia kwa misikiti yote katika ufalme huo, vipaza sauti vitatumika tu wakati wa adhana na iqama na pia sauti inapaswa kuwa kiwango cha chini zaidi iliyvyo hivi sasa.
Kwa mujibu wa gazeti la Gulf News, amri hiyo imetolewa kwa mujibu wa fatwa za wanazuoni maarufu Sheikh Mohammed bin Saleh Al Othaimeen and Saleh Al Fawzan ambao wanasema vipaza sauti vinapaswa kutumika tu wakati wa adhana na iqama.