IQNA

Ibada ya Umrah yafutwa kutokana na hofu ya kirusi cha Corona

11:43 - February 27, 2020
Habari ID: 3472512
TEHRAN (IQNA)- Saudi Arabia imetangaza kusimamisha kwa muda Ibada ya Umrah na Ziyarah katika Msikiti wa Mtume Muhammad SAW mjini Madina kutokana na hofu ya kuenea kirusi cha Corona.

Katika ujumbe wa Twitter mapema Alhamisi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imesema  Ibada ya Umrah imesimamishwa kwa muda ili kuzuia kuenea kirusi cha Corona.

Taarifa hiyo imesema hatua hiyo imechukuliw aili kulinda maisha ya raia na wakazi wa Saudi Arabia na pia wale wanaofika nchini humo kwa ajili ya Umrah au utalii.

Maambukizi ya kirusi cha corona yalianzia katika mji wa Wuhan nchini China Desemba mwaka uliopita wa 2019 na inavyoonesha chanzo chake ni wanyama wasio wa kufuga.

Mbali na mikoa 30 ya China, hivi sasa kirusi hicho kimesambaa kwenye nchi zaidi ya 40 duniani huku watu zaidi ya 81,000 wakiwa wameambukizwa ambapo 78,000 wako nchini China. Aidha n kirusi cha Corona kimeua watu wasiopungua 2,800 ambapo  miongoni mwao 2,717 wako nchini China.

3881784

captcha