IQNA

Mashindano ya Qur'ani Oman kwa ajili ya vijana

14:12 - February 02, 2017
Habari ID: 3470829
IQNA-Mashindano ya 28 ya Qur'ani Tukufu na Hadithi kwa ajili ya vijana katika Ghuba ya Uajemi yatafanyika Muscat, Oman baadaye mwezi huu.

Kwa mujibu wa gazeti la al-Watan, mashindano hayo yatafanyika Februari 25 hadi Machi pili.

Kamati andalizi ya mashindano hayo imekutana hivi karibuni mjini Muscat kujadili nukta mbali mbali za mashindano hayo.

Katika kikao hicho, mkuu wa kamati andalizi Muhammad bin Saed al Munawari na wanachama wengine walijadili njia za kuandaa mashindano bora.

Mashindano ya 28 ya Qur'ani Tukufu na Hadithi kwa ajili ya vijana katika Ghuba ya Uajemi hufanyika kila mwaka katika moja kati ya nchi sita wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi.
Kishikizo: iqna oman
captcha