IQNA

Mazalisho ya Kiislamu katika Intaneti yawe na mvuto

12:03 - September 08, 2015
Habari ID: 3360447
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitizia ulazima wa kuweko mazalisho ya Kiislamu yenye umakini na mvuto kwa ajili ya kutumwa kwenye mitandao ya Intaneti.

Ayatullahil Udhma Khamenei amesema hayo leo wakati alipoonana na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu na wajumbe wa Baraza Kuu la Mitandao ya Intaneti la Iran na huku akiashiria namna mitandao hiyo ilivyo na taathira kubwa katika nyuga tofauti ukiwemo uwanja wa kiutamaduni, kisiasa, kiuchumi, itikadi za kidini na kimaadili amesema, kuna udharura wa kuweko propramu zinazofaa na zinazofanyika kwa umakini mkubwa kwa ajili ya kulinda mipaka ya usalama wa kifikra na kimaadili ya jamii katika mitandao ya Intaneti. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Kuna wajibu wa kutumiwa vizuri uwezo na vipaji vya vijana nchini na kuweka siasa sahihi pamoja na kuchukuliwa hatua makini na zenye uratibu mzuri bila ya kupoteza wakati ili kujitoa katika hali ya kufanya mambo kwa pupa katika uwanja wa mitandao ya Intaneti na kushiriki vilivyo katika uzalishaji wa mambo ya Kiislamu yenye umakini mkubwa na yenye mvuto wa hali ya juu. Ayatullahil Udhma Khamenei ametaja mambo manne ya kuweza kutumika nchini kwa ajili ya kuwa amilifu na kutoa taathira chanya katika mitandao ya Intaneti ambayo ni: Kuwa na marejeo mamoja ya kuchukulia maamuzi, kulipa uzito wa hali ya juu suala la utekelezaji wa maamuzi yanayochukuliwa tena bila ya kupoteza muda, kuweko uratibu wa pamoja baina ya taasisi husika na kujiepusha na mambo ya pembeni na yasiyo muhimu katika suala hilo.../mh

3360206

captcha