IQNA

Al Azhar yataka Waislamu wabadili mitaala ya masomo

16:51 - February 24, 2015
Habari ID: 2891633
Kiongozi wa Chuo Kikuu cha al-Azhar nchini Misri Ahmad al-Tayib, ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kufanyia marekebisho mitalaa ya elimu katika taasisi za elimu ili kupunguza wimbi la vijana kujiunga na makundi ya kigaidi.

Ahmad al-Tayib amesema vijana wengi wa Kiislamu wanaingia kwenye mtego wa makundi yenye misimamo mikali kutokana na ukosefu wa mafunzo ya kutosha kuhusiana na sura sahihi ya Uislamu katika shule nyingi ndani ya nchi za Kiislamu. Amesisitiza kuwa, hali hiyo imetoa mwanya kwa makundi ya kigaidi kutoa mafunzo yaliyopotoshwa kuhusu dini tukufu ya Uislamu.

Sheikh Mkuu wa al-Azhar amesema ukoloni mamboleo duniani pamoja na kupuuzwa utamaduni wa Kiislamu ni sababu nyingine inayowafanya vijana wa Kiislamu kujiunga na makundi ya kigaidi.

“Utamaduni wa Kiislamu umevurugwa na maadui wa dini hii na hii imepelekea vijana kuibuka na misimamo mikali katika nchi za Kiislamu” amesema Ahmad al-Tayib.../mh

2885789

captcha