IQNA

Elimu

Afisa wa Al-Azhar aangazia changamoto katika kutafsiri maandishi ya kidini

11:07 - April 23, 2024
Habari ID: 3478722
IQNA - Naibu mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri amesema kuna changamoto nyingi katika kazi ya tarjuma au tafsiri ya maandiko ya kidini, ikiwa ni pamoja na Qur'ani Tukufu.

Sheikh Mohamed al-Duwaini, akizungumza katika mkutano mjini Cairo, amesema kutafsiri maandishi ya Kiislamu kunahitaji kushinda uwezo wa kukabiliana na changamoto nyingi.

Amesema kazi hii inahitaji ujuzi mwingi, usahihi na ustadi wa hali ya juu, maingiliano na wanazuoni na tahadhari nyingi ili kuepuka upotoshaji wowote katika mchakato wa tafsiri na tarjuma, alisema, Al-Watan iliripoti.

Ama kuhusu tafsiri ya Qur'ani, amesema kuna misemo na istilahi ndani ya Kitabu hicho kitukufu ambazo haziwezi kutafsiriwa katika lugha nyingine.

Pia kuna baadhi ya istilahi katika fikra na sayansi ya Kiislamu, hasa katika Fiqh (sheria za Kiislamu) ambazo hazina mshabaha katika lugha nyinginezo, al-Duwaini alibainisha.

Ndiyo maana kuna haja ya kuwa na maelezo katika tafsiri ili wasomaji wa lugha lengwa waweze kufahamu dhana hizo, aliendelea kusema.

Afisa huyo wa Al-Azhar alisisitiza haja ya kukuza Uislamu kupitia tafsiri sahihi ya maandishi ya Kiislamu, akisema maadui wameanzisha kampeni kubwa ya kuwazuia watu katika nchi za Magharibi kuelewa ukweli wa Uislamu.

Aliongeza kuwa katika ulimwengu wa sasa, ustaarabu unahusika katika makabiliano sio kwa kutumia silaha, lakini kwa kutumia mawazo na ujuzi.

 4211698

Kishikizo: qurani al azhar
captcha