IQNA

Miujiza ya Qur'ani kujadiliwa katika Mkutano wa kimataifa Misri

13:15 - December 26, 2016
Habari ID: 3470761
IQNA-Duru ya tano ya mkutano wa kimataifa wa 'Upeo wa Miujiza ya Qur'ani Tukufu' umepengwa kufanyika mwezi Aprili nchini Misri.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mkutano huo ambao umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Al Azhar utafanyika kuanzia Aprili 25 hadi 27 katika Kitivo cha Lugha ya Kiarabu cha chuo kicho katika mji wa Al Zagazig mkoa wa Al Sharqia.

Kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa Jumuiya ya kImataifa ya Miujiza ya Qur'ani na Sunnah.

Kati ya mada zitakazojadiliwa katika mkutano huo ni miujiza ya Qur'ani kwa mtazamo wa kisayansi, kibalagha, kihistoria, kisheria, kilugha, na kimoflojia.

Lengo kuu la kongamano hilo la kila mwaka ni kuwahimiza wasomi Waislamu kufanya utafiti zaidi kuhusu miujiza ya Qur'ani na Sunnah katika sekta za tiba, uhandisi, biolojia, astronomia, jiolojia, sayansi za kijamii na kidini.

3461752

captcha