IQNA

Maonyesho ya mavazi ya kike ya Kiislamu kufanyika Tokyo+PICHA

13:20 - November 14, 2016
Habari ID: 3470675
IQNA-Maonyesho ya kwanza ya mavazi ya kike ya Kiislamu yamepangwa kufanyika tarehe 22-23 Novemba katika mji wa Tokyo, nchini Japan.
















Kwa mujibu wa gazeti la Japan Times, maonyesho hayo yatakuwa maalumu kwa ajili ya mavazi ya Kiislamu ya Hijabu yanayotumiwa na wanawake Waislamu.

Waandalizi wa maonyesho hayo wanasema sababu kuu ya kuyaandaa ni ongezeko la watalii Waislamu nchini Japan. Mbali na kujitahidi kuimarisha uhusiano wa Japan na nchi za Kiislamu, maonyesho hayo pia yanalenga kuondoa dhana potofu iliyopi kuhusu mavazi ya Kiislamu.

Kwa ujumla kutakuwa na maonyesho manne pamoja na warsha ya miundo ya vazi la Hijabu katika siku hizo mbili.

Maonyesho hayo ya mavazi ya kike ya Kiislamu yatafanyika mjini Tokyo sambamba na maonyesho vya vyakula, bidhaa na huduma Halal.

Zifuatazo ni picha za baadhi ya mitindo ya Hijabu inayotazamiwa kuwasilishwa katika maonyesho hayo.

Maonyesho ya mavazi ya kike ya Kiislamu kufanyika Tokyo+PICHAMaonyesho ya mavazi ya kike ya Kiislamu kufanyika Tokyo+PICHAMaonyesho ya mavazi ya kike ya Kiislamu kufanyika Tokyo+PICHAMaonyesho ya mavazi ya kike ya Kiislamu kufanyika Tokyo+PICHAMaonyesho ya mavazi ya kike ya Kiislamu kufanyika Tokyo+PICHA

3545563

captcha