Sala ya Idul Fitr iliswaliwa katika makaburi mawili matukufu ya Imam Hussein (AS) na Hadhrat Abbas pamoja na katika eneo linalojulikana kama Bain-ul-Haramain, eneo lililo kati ya makaburi hayo mawili matukufu.
Sheikh Ahmed al-Safi aliongoza sala na kutoa khutba katika eneo hilo takatifu, tovuti ya al-Kafeel iliripoti.
Katika khutba zake, Sheikh al-Safi amekosoa ukimya wa nchi na vyombo vya habari vya dunia kuhusu jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wa Palestina hasa katika Ukanda wa Gaza.
Vile vile ameukosoa Umoja wa Mataifa kwa kufanya lolote kusimamisha mauaji ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina na kurejesha haki za watu wa Palestina.
Hapo awali ofisi ya Ayatullah Ali al-Sistani, kiongozi mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq, ilitangaza Jumatano kuwa Idul Fitr katika nchi hiyo ya Kiarabu.
4209810