IQNA

Umrah na Ramadhani

Madina: Msikiti wa Mtume wapokea Waislamu milioni 15 katika nusu ya kwanza ya Ramadhani

15:58 - March 29, 2024
Habari ID: 3478601
IQNA - Katika nusu ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, karibu Waislamu milioni 15 walikwenda kwenye Msikiti wa Mtume SAW yaani Al-Masjid an-Nabawi huko Madina, eneo la pili takatifu katika Uislamu, kulingana na afisa wa Saudia.

Wageni hao walilakiwa na mtandao wa huduma "uliopangwa vyema", alisema Sultan Al Badri, Mkuu wa Takwimu na Habari katika Mamlaka ya Utunzaji na Usimamizi wa Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina.

Al Badri amesema karibu waumini 500,000 walipata vibali kupitia jukwaa la kielektroniki la Nusuk kuswali katika Al Rawda Al Sharifa, eneo ambalo liko ndani ya msikiti huo na liliko kaburi la Mtume Muhammad (SAW). Alisema kuwa vibali vya Nusuk vimeboresha usimamizi na uingiaji wa umati, kama ilivyoripotiwa na TV ya Saudi Al Ekhbariya.

Mwezi wa Ramadhani ni msimu wa kilele cha Umrah, au hija ndogo, kwenye Msikiti Mkuu yaani Masjid al Haram huko Makka, mahali patakatifu zaidi katika Uislamu. Kufuatia kukamilika kwa Umra, mahujaji wengi husafiri kwenda Madina kuswali katika Msikiti wa Mtume na kutembelea maeneo mengine ya Kiislamu mjini humo.

Mamlaka ya Saudia inayohusika na Msikiti wa Mtume (SAW) imeeleza kujiandaa kwao kuhudumia wimbi kubwa la Waislamu wanaotembelea eneo hilo wakati wa Ramadhani, mwezi ambao Waislamu hukithirisha ibada. Inakadiriwa kuwa zaidi ya milo milioni 8.5 ya futari itagawiwa kwa waumini wanaofunga mwaka huu.

Kulingana na data rasmi, zaidi ya Waislamu milioni 280 walisali katika Msikiti wa Mtume mnamo 2023.

3487742

Habari zinazohusiana
captcha