IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Qur’ani ya Afrika yafanyika Tanzania

14:14 - March 27, 2024
Habari ID: 3478590
IQNA- Fainali za 24 za Mashindano ya Quran Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al Hikma Foundation kwa kushirikisha nchi mbalimbali 22 za Afrika na nje ya Afrika yamefanyika kwa mafanikio katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania Machi 24, 2024.

Mshindi wa kwanza wa Mashindano hayo alikuwa  ni Ibrahim Sow wa Ivory Coast aliyepata shilingi za Tanzania milioni 27, mshindi wa pili Haafith Abdulkariim Kabiito kutoka Uganda shilingi milioni 17.2 , mshindi wa tatu Kamil Almin Swaleh kutoka Tanzania shilingi milioni 11.6 , mshindi wa nne Kamilou Koura kutoka Togo shilingi milioni 8.1 na mshindi wa tano Idris Nshimwe kutoka Burundi shilingi milioni 4.5.

Akizungumza katika sherehe za kuwatunuku washindi zawadi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza waumini wa dini ya Kiislamu kuendelea kuhifadhi Qur’ani Tukufu na kufundisha watoto wao kuisoma na pia wazidishe kutoa sadaka kwa watu wenye mahitaji hususani katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano na kuzidi kupiga hatua za maendeleo nchini.

Aidha Dk.Mwinyi ameipongeza Taasisi ya Al Hikma Foundation kwa kuandaa mashindano hayo makubwa ambayo yanaitangaza Tanzania kwa kushirikisha nchi mbalimbali.

4207166

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

captcha