IQNA

Pepo Katika Qur'ani /2

Maelezo ya Qur'ani Tukufu kuhusu Pepo: Bustani ambazo mito inapita chini yake

13:32 - February 01, 2024
Habari ID: 3478285
IQNA – Wakati uzuri wa pepo hauelezeki au kudirikiwa kikamilifu na mwanadamu, Qur'ani Tukufu inailinganisha na mandhari ya ajabu katika dunia hii ambayo daima ni ya kijani kibichi na yenye shime na mito ya maji safi ambayo inapita chini ya bustani zake.

Kuna aya nyingi katika Qur'ani  zinazozungumzia pepo na watu wa peponi. Katika Aya ya 11 ya Surah Al-Buruj, Qur'ani inaielezea hivi:

“Hakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa."

Pia kuna maelezo kama hayo katika Aya ya 198 ya Surah Al Imran:

" Lakini walio mcha Mola wao Mlezi watapata Mabustani yanayo pita mito kati yake. Watadumu humo. Hayo ni makaribisho yao yatokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na vilioko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kwa watu wema."

Soma Zaidi:

Kudiriki baraka za Peponi ni zaidi ya uwezo wa ufahamu wa mwanadamu

Ikilinganishwa na ulimwengu huu, pepo inafafanuliwa kuwa bustani zilizojaa miti na kijani kibichi. “Na mabustani yenye miti iliyo kamatana.” (Aya ya 16 ya Surah An-Naba)

Pepo inaitwa Jannah kwa Kiarabu kwani ina majani mazito ambayo kivuli chake ni cha milele.

" Mfano wa Bustani waliyo ahidiwa wachamngu, kati yake inapita mito, matunda yake ni ya daima, na pia kivuli chake. Huu ndio mwisho wa wale walio walio jilinda... (Aya ya 35 ya Surah Ar-Raad)

Katika aya nyingine, Qur'ani inazungumza kuhusu mito, chemchem na baraka nyingi katika bustani hizi:

" Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem." (Aya ya 15 ya Surah Adh-Dhariyat)

" Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito. " (Aya ya 54 ya Surah Al-Qamar)

"Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na neema." (Aya ya 17 ya Surah At-Tur)

captcha