IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia)

Msikiti washambuliwa mara ya nne katika siku 10 nchini Marekani

22:14 - July 07, 2023
Habari ID: 3477249
WASHINGTON, DC (IQNA)-Msikiti huko Portales, New Mexico, nchini Marekani umeharibiwa kwa mara ya nne katika kipindi cha siku 10 huku polisi wakipuuza hawajazingatia mashambulio hayo yanayorudiwa, ambayo ni pamoja na kuvunjia heshima Qur’ani Tukufu.

Shambulio la hivi karibuni la Alhamisi limesababisha shirika kubwa zaidi la haki za raia na utetezi wa Waislamu Marekani, Baraza juu ya Mahusiano ya Amerika na Kiisilamu (CAIR), kutaka uchunguzi ufanyike.

Siku ya Alhamisi, Msikiti wa Portales ulilwengwa tena kwa maandishi yenye chuki dhidi ya ukutani. Benssouda, ambaye anasimamia msikiti huo, alisema alihisi kutokuheshimiwa na kukiukwa na mashambulio ya mara kwa mara, sio tu kama Mwislamu bali pia kama mwanajamii katika eneo  hilo.

Msikiti huo ulipata hasara ya maelfu ya dola katika uharibifu baada ya wahalifu kuvunja ndani ya jengo hilo wiki iliyopita na kuvunjia heshima nakala za Qur’ani Tukufu. "

Wakati huo huo, polisi wanasema uharibifu huo ni "sawa na ile kwenye majengo mengine ya wazi" na ni " sio uhalifu wa chuki."

Hivi karibuni CAIR ilibaini katika ripoti kwamba, Chuki dhidi ya Uislamu imeongezeka mara tatu Marekani tokea hujuma za Septemba11 mwaka 2001 huku wanasiasa wakiitumia wakitumia chuki hiyo kuendeleza ajenda zao wenyewe.

3484240

Habari zinazohusiana
captcha