IQNA

Mbinu ya Elimu ya Manabii; Ibrahim / 10

Mizani ya kutathmini wanadamu

10:51 - July 02, 2023
Habari ID: 3477226
TEHRAN (IQNA) – Katika kuchunguza vitabu vilivyoandikwa kuhusu mbinu na kanuni za elimu, tunakumbana na kiasi kikubwa cha mbinu za elimu na katika mbinu zote hizo, majaribio na mitihani ni njia muhimu kwa elimu.

Kuwatahini watu binafsi ni mojawapo ya mbinu za elimu. Katika njia hii, mwalimu huweka mwanafunzi katika hali ya kumuwezesha kuonyesha thamani na sifa zake. Nabii Ibrahim (AS), ambaye alikuwa nabii Ulul Azm, alitumia njia hii ambayo Mwenyezi Mungu anataja hili katika Qur'ani Tukufu.

Kupima au kutahini ni njia mojawapo bora ya kielimu na hata Mwenyezi Mungu anasema ndani ya Quran kuwa anawajaribu wanadamu. Kujaribu huwapa changamoto wanadamu. Kwa mfano, watu wanapaswa kujifunza kanuni za trafiki ili wawe madereva lakini haitoshi. Wanapaswa pia kuendesha gari kwa muda ili kujijaribu na kujifunza kila kitu.

Katika Qur'ani Tukufu, Nabii Ibrahim (AS) ametambulishwa kama baba ambaye anamtahini mtoto wake:

“ ‘Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri." (Aya ya 102 ya Surah As-Saffat)

Kwa mujibu wa aya hii, Nabii Ibrahim (AS) aliuliza maoni ya mwanawe na inaweza kuwa kwa sababu mbili:

1-Ushauri nasaha 2-kutahini.

Ni wazi kwamba mtu hatafuti ushauri kwa jambo ambalo Mwenyez Mungu ameamuru. Kwa hivyo  nukta ya kwanza si sahili. Ama ya pili, kuna maelezo katika tafsiri ya Qur'ani Tukufu:

Allamah Tabatabai anasema katika Tafsisi ya Qur'ani ya Al-Mizan kwamba neno la Kiarabu 'Tara' katika aya hiyo linamaanisha "nini maoni yako (kuhusu hili)" sio "unaona nini". Ibrahimu (AS) alimjaribu mwanawe ili kuona majibu yake ni nini.

Kwa mujibu wa tafsiri ya Qur'ani ya Athna Ashari, Nabii Ibrahim hakuomba mashauriano bali alimuuliza Ismail (AS) mtazamo wake kuona kama anaweza kufaulu mtihani huu mkubwa au la kuhusu subira na uthabiti au istikma

Ismail (AS) alipita mtihani huu kwa fahari na akatenda kwa mujibu wa amri ya Mwenyezi Mungu na hivyo alitii amri yake.

captcha