IQNA

Maadili katika Qur'ani / 4

Moto unaounguza mtu mwenye matamanio ya nafsi yenye kufurut ada

20:18 - June 11, 2023
Habari ID: 3477131
Watu wenye hamu sana ya kusonga mbili wakati mwingine hutumia vibaya hisia za wengine kufikia madaraka na matamanio yao mengine.

Katika baadhi ya hadithi za Qur'ani Tukufu, kuna watu wenye sifa hii ambao wamejipotosha wenyewe na pia kuwapotosha wengine.

Kuwa na tamaa kubwa ni jambo la hatari kwa mtu binafsi na jamii. Wale wenye tamaa ya kupita kiasi wanatafuta kuitawala jamii na kutaka watu wawafuate.

Kama vile wengine wanavyotumia pesa zao kufikia malengo ya kilimwengu yawe mazuri au mabaya, watu wenye tamaa ya kupita kiasi hutumia hisia za watu kufikia mamlaka na miradi mingine ya kilimwengu.

Ingawa watu kama hao wanaweza kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri au uwezo wa juu na vipawa vya kuwatawala watu, hawako huru kutokana na makosa na dosari walizonazo

Kwa sababu mtazamo wao wa kuzingatia ni ulimwengu huu, sio akhera, matamanio na malengo yao ya kidunia huwafanya wachukue maamuzi ambayo hayawaelekezi wao wenyewe tu bali pia wengine kwenye njia mbaya na kuelekea maangamizi.

Imamu Sadiq (AS) anatutahadharisha kuwa tusiwafuate watu kama hao wanaotafuta utawala na madaraka kwa sababu wanajisababishia wao wenyewe na wengine kupotea.

Quran Tukufu inawataja baadhi ya watu hawa:

“Na Firauni alitangaza kwa watu wake, akisema: Enyi watu wangu! Kwani mimi sinao huu ufalme wa Misri, na hii mito inapita chini yangu? Je! Hamwoni?  Au mimi si bora kuliko huyu aliye mnyonge, wala hawezi kusema waziwazi? ” (Aya 50-51 za Surah Zukhruf)

Aya hizi zinaonyesha kiburi cha Firauni na tamaa kubwa kupita kiasi aliyokuwa nayo. Alijua kwamba Musa (AS) alikuwa sahihi na alikuwa ametumwa na Mungu, lakini aliwadanganya watu na kujidai kuwa mungu kwa sababu alipenda mamlaka na kutawala watu.

Farao akajiongoza yeye na wale waliokuwa pamoja naye hukumu ya milele. “Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itapo fika Saa ya Kiyama patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!” ( Aya ya 46 ya Surat Ghafir).

captcha