IQNA

Michezo na Waislamu

Picha aliyosambaza Haaland kuhusu msikiti maarufu UAE yaibua gumzo kuhusu dini yake

21:25 - December 12, 2022
Habari ID: 3476239
TEHRAN (IQNA) – Nyota wa soka wa Norway Erling Haaland amesambaza picha za Msikiti Mkuu wa Sheikh Zayed huko Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na kuzua gumzo uvumi kuhusu dini yake.

Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 22 alichapisha picha mbili za msikiti huo kwenye akaunti yake ya Instagram, na kuandika"Wow" katika kuusifu eneo hilo la ibada

Alikuwa Abu Dhabi kama sehemu ya kambi ya mazoezi ya Manchester City.

Kwa mujibu wa vyombo kadhaa vya habari vya Kiarabu, picha hiyo iliyosambazwa na mchezaji huyo imesababisha uvumi kuhusu dini yake kwenye mitandao ya kijamii.

Hii si mara ya kwanza kwa dini ya Haaland kuwa chanzo cha mjadala miongoni mwa watumiaji wa mtandao.

Mnamo Septemba 2021, Haaland alisherehekea bao na mwenzake wa wakati huo, Mahmoud Dahoud. Akaunti rasmi ya Twitter ya Borussia Dortmund ilichapisha picha ya Dahoud ikiwa na maelezo yasemayo, "Alhamdulillah Habibi." Kilichovutia umakini wa wengi ni jibu la Erling ambaye aliandika, "Alhamdulillah."

Wengi hapo awali walidhani Haaland alikuwa akiheshimu dini na imani ya rafiki yake na mwanasoka mwenzake. Hata hivyo, hiyo haikuwa mara ya pekee ujumbe wake wa Twitter kuwafanya mashabiki kuamini kuwa yeye ni Mwislamu.

Mapema mwaka huu, Haaland alijiunga na Manchester City. Ilimbidi kusubiri wiki chache kabla ya kuichezea klabu hiyo kwa mara ya kwanza tangu alipojiunga mwanzoni mwa dirisha la uhamisho. Wakati akaunti ya Twitter yenye makao yake makuu mjini Man City ilipomtakia heri ya kuzaliwa tarehe 21 Julai, alijibu, “Asante! Mechi ya kwanza ni dhidi ya Bayern Inshallah.”

Sasa, wengi wangefikiri kwamba alikuwa akimtuza tu rafiki yake mara ya kwanza alipoandika kwenye Twitter "Alhamdulillah". Lakini mara ya pili, alipotaja “Inshallah”, istilahi maarufu ya Kiislamu ambayo ina maana ya “Mungu akipenda,” iliwashangaza mashabiki kwani hakuna aliyetarajia Haaland kuwa Muislamu..

Pamoja na hayo yote yamkini Erling ni mtu ambaye anaheshimu na anapenda Uislamu lakini sio muumini. Aidha, hajadhihirisha hadharani dini na imani yake.

4106459

captcha