Katika siku ya kwanza ya finali hizo kulikuwa na washiriki 13 kutoka Indonesia, Mauritania, Nigeria, Ivory Coast, Chad, Burundi, Iran, Uganda, Pakistan, Senegal, Gambia, na Afghanistan.
Majaji katika kitengo cha wanawake ni kutoka Iran, Jordan, Iraq, Syria, Indonesia na Malaysia.
Mashindano ya 37 Kimataifa ya Qur’ani ya Iran yalianza Jumamosi 6 Machi na yanatazamiwa kumalizika Alhamisi 11 Macho.
Kauli mbiu ya mashindano ya mwaka huu ni 'Kitabu Kimoja, Ummah Mmoja".
Mashindano ya mwaka huu ni ya kipekee kwani kutokana na janga la COVID-19 au corona, yanafanyika kwa njia ya Intaneti.
Zaidi watazamaji milioni 2.5 walifuatilia duru za mchujo za mashindano hayo kwa njia ya intaneti na inatazamiwa kuwa baina ya watu milioni 6-8 watafuatilia fainali ya mashindano hayo kwa njia ya intaneti.