IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Dua za Kila Siku za Mwezi wa Ramadhani- Siku ya 18

Dua hizi za kila siku za Mwezi wa Ramadhani husomwa toka mwanzo ya tarehe mosi Ramadhani hadi siku ya mwisho katika mwezi huu mtukufu. Kila dua ina siku yake, na inaweza kusomwa mara nyingi kadiri ya uwezo wa mtu mwenyewe.

Ee Mwenyezi Mungu! Nizindushe katika mwezi huu ili nipate baraka za masiku yake, Uninawirishe moyo wangu kwa mwangaza wa nuru zake (Nuru za mwezi huu wa Ramadhani) Uvishike viungo vyangu vyote viwe ni vyenye kufuata nyayo zake, kwa Nuru yako ewe Mwangaza wa nyoyo za wakujuao.

Kishikizo: dua za kila siku ، ramadhani