IQNA

Qur'ani Tukufu

Wahifadhi Qur'ani watunukiwa zawadi nchini Ghana

19:07 - May 06, 2023
Habari ID: 3476963
TEHRAN (IQNA) - Hafla imefanyika katika mji mkuu wa Ghana wa Accra kuwaenzi washindi wa shindano la kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Msikiti wa Al-Haji Nurgah katika kitongoji cha Mji Mpya wa Accra uliandaa hafla hiyo.

Mashindano hayo yameandaliwa na Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Ghana kwa ushirikiano na Taasisi ya Elimu ya Kiislamu ya nchi hiyo ya Kiafrika kwa lengo la kukuza kujifunza Qur'ani miongoni mwa vijana.

Kuhifadhi Qur'ani nzima, kuhifadhi nusu ya Qur'ani na kuhifadhi Juzuu ya 30  ni kategoria zilizokuwa katika shindano hilo.

Wataalamu wa Qur'ani Tukufu katika nyanja za kuhifadhi, Tajweed, na Lahn walitathmini maonyesho ya washindani na kutangaza washindi.

Washiriki watatu bora katika kila kategoria walitunukiwa katika hafla hiyo ya heshima.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Ghana, Saleh Dagheleh, qari wa Iran aliyetumwa katika nchi hiyo ya Kiafrika kwa ajili ya kusoma Qur'ani, Sheikh Mustafa Yajalal, Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Kiislamu, na idadi kadhaa ya shakhsia na maafisa wa kidini.

Quran Memorizer Awarded in Ghana

Quran Memorizer Awarded in Ghana

3483457

captcha