IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Tuzo ya Qur’ani Tukufu ya Ras Al Khaimah yahitimishwa

22:32 - February 19, 2023
Habari ID: 3476585
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya 21 ya Tuzo ya Qur’ani ya Ras Al Khaimah yamehitimishwa huko Ras Al Khaimah, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Mashindano hayo yalifadhiliwa na Sheikh Saud bin Saqr Al Qasimi, tovuti ya Al-Ittihad iliripoti.

Kando ya mashindano hayo ya Qur'ani kulikuwa na warsha, hotuba, vikao vya kielimu na vipindi vya redio katika misikiti, shule, vyuo na vituo vya kitamaduni huko Ras Al-Khaimah.

Ahmed Muhammad al-Shahi, Mkuu wa Wakfu wa Ras Al Khaimah wa Qur'ani Tukufu na Sayansi Zake amesema katika hafla hiyo ya kuhitimisha kuwa waandaji wa Tuzo ya Qur'ani ya Ras Al Khaimah wanataka kuhimiza ustahimilivu, subira na maadili mema miongoni mwa vijana sambamba na kuwahimiza kukuza vipaji vyao.

Mashindano hayo yalifanyika kwa makundi tofauti ya washiriki wakiwemo wavulana, wasichana, wanawake, maimamu wa misikiti, waadhini, wafungwa na Waislamu wapya wanaoishi UAE.

Washindi walitunukiwa zawadi za pesa taslimu ambazo zilikuwa jumla ya zaidi ya dirham 575,000 za UAE.

4122940

captcha