IQNA

Watoto Wapalestina katika jela za kuogofya za Israel wazidi kuongezeka

17:34 - April 24, 2016
Habari ID: 3470267
Idadi ya watoto wadogo wa Kipalestina wanaozuiliwa katika jela za kuogofya za utawala wa kizayuni wa Israel imeongezeka kwa kiwango kikubwa tangu Oktoba mwaka uliopita wa 2015.

Gazeti la kizayuni la Haaretz limeripoti kuwa, idadi ya wafungwa wa Kipalestina ambao ni watoto wadogo katika jela hizo imeongezeka kutoka 170 Septemba mwaka uliopita wa 2015, hadi 438 Januari mwaka huu wa 2016.

Takwimu za Shirika la Magereza la Israel zimeonyesha kuwa, idadi ya wafungwa Wapalestina wenye umri kati ya miaka 16-18 imeongezeka kutoka 143 hadi 324 katika kipindi hicho, huku walio na umri wa miaka 14-16 pia ikiongezeka kutoka 27 hadi 98. Aidha binti wa miaka 12 wa Kipalestina ndiye mfungwa mwenye umri mdogo zaidi katika korokoro za kuogofya za utawala huo haramu. Utawala ghasibu wa Israel ulishadidisha hujuma na kamata kamata zake dhidi ya Wapalestina, tangu waanzishe Intifadha ya Quds Oktoba mwaka jana.

Mbali na wafungwa 7,000 wa Kipalestina, utawala wa Kizayuni pia unawashikilia zaidi ya wafungwa 5,000 wa kigeni katika mazingira magumu na ya kutisha.

3459611

captcha