IQNA

Sayyid Hassan Nasrullah

Kuuawa shahidi ni silaha imara zaidi mbele ya adui

18:30 - November 12, 2015
Habari ID: 3447507
Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, moyo wa kutaka shahada na kuuawa shahidi daima ni silaha imara zaidi mbele ya adui.

Sayyid Nasrullah aliyasema hayo jana katika maadhimisho ya “Siku ya Shahidi” huko Beirut Lebanon ambapo sambamba na kuwaenzi mashahidi kutokana na kujitolea kwao uhai wao na maisha yao amesema kuwa, daima watu wanapaswa kukumbuka kujitolea huku kwa mashahidi. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema na hapa ninamnukuu:

“Wakati tunapozungumzia ushindi tofauti, tunapaswa kukumbuka kwamba, ushindi huu umepatikana kwa baraka za damu toharifu za mashahidi.” Mwisho wa kunukuu. Akihutubia katika maadhimisho hayo ya Siku ya Shahidi, Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema pia kwamba, matunda bora kabisa ya damu za mashahidi ni kwamba, wao wameyapatia mataifa moyo wa jihadi, muqawama, heshima, utukufu na kupambana na madhila na wakati huo huo kuleta mwamko wa kimaanawi. Sayyid Nasrullah amezungumzia pia matukio ya Palestina na kubainisha kwamba, endapo Wapalestina watadumisha umoja na mshikamano wao, katu utawala wa Kizayuni wa Israel hauwezi kukabiliana na mapambano na kusimama kidete kwa Wapalestina.

3447458

captcha