IQNA

Utawala wa Kizayuni waua shahidi Wapalestina 46 mwezi Oktoba

20:37 - October 19, 2015
Habari ID: 3390450
Jeshi la Israel limewaua shahidi Wapalestina wapatao 46 tangu kuanza Intifadha au mwamko mpya mapema mwezi huu wa Oktoba.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, Wapalestina hao wameuawa huko Ukanda wa Ghaza, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds Tukufu katika mapambano na Wazayuni na askari wa utawala haramu wa Israel.

Wakati huio huo, Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas Hessam Badran amesema oparesheni za kujitolea kufa shahidi za Wapalestina dhidi ya Wazayuni ni jibu kwa jinai za utawala wa Israel na walowezi wa Kizayuni. Amesema vijana mabingwa wa Kipalestina wamefanikiwa kupenya katika kitovu cha utawala wa Kizayuni na kutekeleza oparesheni.

Moto wa wimbi jipya la mapambano kati ya Wapalestina na Wazayuni uliripuka tarehe Mosi ya mwezi huu wa Oktoba kutokana na kitendo cha kichochezi cha askari wa utawala haramu wa Israel cha kuwawekea mipaka na vizuizi Waislamu wa Palestina kuingia msikiti mtukufu wa Al-Aqsa pamoja na hatua ya kichokozi ya Waziri wa Kilimo wa utawala huo ghasibu, akiandamana na makumi ya walowezi wa Kizayuni ya kuingia ndani ya msikiti huo.../mh

3389251

captcha