IQNA

Muirani ashika nafasi ya kwanza mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Russia

16:55 - October 12, 2015
Habari ID: 3384686
Musa Motamedi hafidh wa Qur’ani kutoka Iran ameshika nafasi ya kwanza katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani katika mji mkuu wa Russia, Moscow.

Motamedi ambaye alishiriki katika kitengo cha kuhifadhi Qur’ani kikamilifu alpata nafasi ya kwanza huku washiriki wa Yemen na Tanzania wakishika nafasi za pili na tatu kwa taratibu.
Motamedi alizaliwa mwaka 1988 katika mji mtakatifu wa Qom na alipata nafasi ya pili katika mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur’ani mwaka 2013.
Zaidi ya watu 6,000 wakiwemo mamufti kutoka maeneo mbali mbali ya Russia na mabalozi wa nchi za Waislamu walishiriki katika sherehe za kuwatunuku zawadi washiriki Jumapili usiku.
Washindi walipata zawadi za fedha taslimu US$10,000, US$7,000 na US$3,000 kwa taratibu.
Kulikuwa na washiriki kutoka nchi 44 ambapo mashindano hayo yalianza Oktoba 9-11. Majaji katika mashindano hayo walikuwa ni watalamu wa Qur’ani kutoka Jordan, Russia, Brunei, Misri na Yemen.

3384252

captcha