IQNA

Rambirambi baada ya kuuawa shahidi Jenerali Muirani vitani Syria

22:00 - October 09, 2015
Habari ID: 3383361
Rais wa Iran na Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu wametoa ujumbe tofauti kufuatia kuuawa shahidi Brigedia Jenerali Hussein Hamedani katika vita dhidi ya magaidi na kutoa mkono wa pole kwa wananchi wa Iran.

Rais Hassan Rouhani wa Iran amesisitiza katika ujumbe aliotoa leo kufuatia kuuawa shahidi Brigedia Jenerali Hamedani kuwa, kuuliwa shahidi mpiganaji huyo asiyechoka ambaye alimuitikia Mola wake wakati akitekeleza kazi ya ushauri kwa ajili ya kuimarisha harakati ya muqawama wa Kiislamu katika vita dhidi ya kundi la kigaidi la ISIS au Daesh na waungaji mkono wake, kumesababisha hasara na huzuni kubwa.

Katika ujumbe huo, Rais wa Iran amebainisha kuwa kufa shahidi si aina ya mauti, bali ni saada na uhai endelelevu, ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaahidi waja wake maalumu. Rais Hassan Rouhani amemuomba Mola awape subira wapiganaji wenzake shahidi Hamedani na kuwapa uvumilivu na malipo familia ya shahidi huyo wa daraja ya juu. Wakati huo huo Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ametoa ujumbe kwa mnasaba huo na kueleza kuwa Shahidi Brigedia Jenerali Hussein Hamedan ametekeleza juhudi za dhati katika nyanja ngumu na katika kulinda na kutetea malengo ya Uislamu na ya Mapinduzi. Brigedia Jenerali Hussein Hamedani ambaye alikuwa mmoja wa makamanda wa kipindi cha vita vya Kujitetea Kutakatifu na Mshauri wa ngazi ya juu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, jana alasiri  aliuliwa shahidi na magaidi wa Daesh huko katika kitongoji kimoja katika mji wa Halab wakati akitekeleza majukumu ya ushauri.

captcha