IQNA

Warsha

Kikao cha Webinar Nairobi chajadili Nafasi ya Wanawake kwa Mtazamo wa Qur'ani

15:14 - May 31, 2023
Habari ID: 3477074
TEHRAN (IQNA) – Semina ya mtandaoni ilifanyika nchini Kenya hivi karibuni ili kujadili hali ya kisheria ya wanawake katika familia na jamii kwa mtazamo wa Qur'ani Tukufu na dini zingine.

Kituo cha Utamaduni cha Iran katika nchi hiyo ya Kiafrika kiliandaa hafla hiyo kwa ushirikiano na kitivo cha falsafa na masomo ya kidini cha Chuo Kikuu cha Nairobi.

Wasomi kutoka vyuo vikuu nchini Kenya na Iran walihutubia kikao hicho cha mtandaoni, kwa mujibu wa Shirika la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu (ICRO).

Katika hotuba yake, Mwambata wa Utamaduni wa Iran Mohammad Reza Khatibi Vala amesema warsha hiyo  inalenga kuzungumzia mafundisho ya kina ya imani tofauti kuhusu nafasi na hadhi ya mwanamke.

Aliongeza kuwa utafiti wa vitabu vitakatifu na maandishi ya kidini husaidia mtu kupata ufahamu wa kina wa kanuni zinazoongoza mwenendo wa wanawake katika mifumo ya kidini.

Profesa wa chuo kikuu cha Iran, Fereshteh Rouhafza katika hotuba yake aliashiria aya ya 97 ya Surah An-Nahl ya Qur'ani Tukufu na kusema aya hii na nyingine nyingi Qur'ani Tukufu zimebainisha adhama na hadhi ya wanaume na wanawake.

Alibainisha kuwa kwa mujibu wa aya hiyo, Mwenyezi Mungu huwapa thawabu waumini wanaofanya mambo mema bila kujali jinsia zao.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Nairobi Hassan Kinyua, ambaye ana Shahada ya Uzamivu au PhD katika masomo ya kidini, alikuwa mzungumzaji mwingine katika semina hiyo.

Alizungumzia Uislamu na haki za wanawake, akibainisha kuwa kuna Sura nzima ya Qur'ani Tukufu, Surah An-Nisa, iliyopewa jina la wanawake, ambayo inaonyesha jinsi Uislamu unavyomheshimu na kuthamini wanawake.

Aliitaja Siira ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) kuwa ni mfano bora unaoonyesha jinsi haki za wanawake zinavyoheshimiwa katika Uislamu.

Wazungumzaji wengine pia walifafanua juu ya mada kama vile mchango na nafasi ya wanawake katika nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi, haki za wanawake, usawa wa kijinsia, na kuwatendea vyema wanawake kwa mujibu wa mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

4144733

captcha