IQNA

Mazungumzo ya Kidini

Papa Francis, Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Ulimwenguni wakutana mjini Vatican

17:23 - May 28, 2023
Habari ID: 3477062
TEHRAN (IQNA) - Siku ya Jumamosi, Papa Francis Kiongozi wa Kanisa Katoloji Duniani alikutana na Sheikh Mohammad Al-Issa, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Ulimwenguni (MWL), katika ofisi yake katika Jumba la Saint Martha huko Vatican.

Walijadili masuala mbalimbali yanayohusiana na maadili ya kawaida na muungano wa ustaarabu.Baada ya mkutano huo, Alissa alionyesha furaha yake kwa mazungumzo ya uaminifu, ya kindugu na ya kina na Papa Francis kwenye makazi yake.
Alisema: "Tulizungumza kuhusu maadili yetu ya pamoja na kujenga madaraja kati ya ustaarabu kulingana na mipango madhubuti na endelevu. Ninathamini ukarimu wa Papa Francis na hisia za kiungwana."
Papa Francis alianza tena ratiba yake ya kawaida Jumamosi na alikuwa na mikutano kadhaa ya faragha, baada ya kusitisha mikutano siku ya Ijumaa kutokana na homa.

3483728

captcha