IQNA

Kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la Waislamu Ujerumani

8:55 - May 01, 2021
Habari ID: 3473865
TEHRAN (IQNA)- Uchunguzi mpya unaonyesha kuwa, miaka ya hivi karibuni imeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya Waislamu nchini Ujerumani

Uchunguzi ulifanywa na Idara ya Uhamiaji na Wakimbizi ya Ujerumani kwa kushirikiana an Wizara ya Mambo ya ndani ya Ujerumani chini ya anwani isemayo: "Maisha ya Waislamu nchini Ujerumani mwaka 2020" unaonyesha kuwa, kuna Waislamu milioni 5.3 hadi milioni 5.6 nchini humo na kwamba kiasi hicho ni sawa na asilimia 6.4 hadi 6.7 ya jamii yote ya Wajerumani.

Utafiti huo unasema idadi ya Waislamu nchini Ujerumani imeongezeka kwa watu laki tisa ikilinganishwa na matokeo ya uchunguzi uliofanyika mwaka 2015.

Idadi ya Waislamu wenye asili ya Uturuki nchini Ujerumani inafikia milioni 2.5 sawa na asilimia 45 ya Waislamu wote wa nchi hiyo.

Utafiti huo pia unaonyesha kuwa Waislamu milioni 1.5 wa Ujerumani waliwasili nchini humo kutokea katika nchi zinazozungumza lugha ya Kiarabu wakiwemo asilimia 19 kutoka Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika.

Uchunguzi uliofanywa na kituo cha utafiti cha Pew Research Center cha Marekani unaonyesha kuwa, Uislamu ndiyo dini kubwa inayokuwa na kuongezeka kwa kasi duniani ikilinganishwa na dini nyingine.

Kituo hicho cha utafiti cha Marekani kimesema katika ripoti yake kwamba, hadi kufikia mwaka 2070, Uislamu utakuwa ndiyo dini kubwa zaidi ulimwenguni.

Ujerumani sasa ni nchi ya pili kwa idadi ya Waislamu Ulaya Magharibi baada ya Ufaransa.

3968187

Kishikizo: ujerumani waislamu
captcha