IQNA

Msahafu mkubwa zaidi Indonesia wavutia wengi mwezi wa Ramadhani

19:33 - April 30, 2021
Habari ID: 3473863
TEHRAN (IQNA)- Msahafu wenye kuvunja rekodi kwa ukubwa wake umewekwa katika maonyesho katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta.

Kwa mujibu wa taarifa, Msahafu huo ulitayarishwa na wanafunzi mwaka 2001 na umeweza kuwavutia wengi katika Kituo cha Kiislamu cha Jakarta.

Msahafu huo una urefu wa mita moja na upana wa sentimeta 50 na ulitayarishwa na wanafunzi Chuo Kikuu cha Sayansi za Qur’ani katika eneo la Java ya Kati.

Katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Waislamu kote duniani hujikurubisha zaidi na Qur’ani tukufu na kwa msingi huo mbali na kusoma pia hufanyika maonyesho ya Qur’anin katika nchi mbali mbali.

3474586

captcha