IQNA

Safari ya ujumbe wa Al-Azhar nchini Iran miaka 50 iliyopita + Picha

13:21 - April 29, 2021
Habari ID: 3473860
TEHRAN (IQNA) – Ujumbe wa ngazi za juu wa wanazuoni kutoka Chuo cha Kiislamu cha Al Azhar cha Misri ulitembelea Iran nusu karne iliyopita ikiwa ni katika jitihada za wanazuoni wa Shia na Sunni kuleta umoja wa Kiislamu na ukuruba wa madhehebu.

Katika mahojiano na IQNA, Gholam Reza Amirkhani mtaalamu katika Maktaba ya Kitaifa na Makavazi ya Iran amesema safari hiyo ilikuwa ya kihistoria katika uhusiano wa Iran na Misri.

Amesema mwanazuoni wa ngazi za juu wa Kishia kutoka Iran Ayatullah Mohammad Taqi Qomi ambaye alikuwa amehamia Misri miaka kadhaa kabla ya safari hiyo, alijitahidi sana kustawisha uhusiano na ukuruba baina ya madhebu za Kiislamu.

Ayatullah Qomi alianzisha kituo kilichojulikana kama Dar al-Taqrib kwa lengo la kukurubisha madhehebu za Kiislamu ambapo aliwashirikisha wawakilishi wa madhehebu nne za Ahul Sunna. Amirkhani amesema harakati hizo za Ayatullah Qomi ziliungwa mkono na wanazuoni wa ngazi za juu wa Iran na Misri wakati huo akiwemo Ayatullah Borujerdi na Shekhe mkuu wa Al Azhar Sheikh Mahmoud Shaltut.

Ni kutokana na jitihada hizo ndio ujumbe wa Al Azhar ukafunga safari hadi Iran na kukutana na wanazuoni waandamizi wa Kishia nchini Iran katika miji ya Tehran, Mashhad, Qom na Isfahan.

Ujumbe huo uliandamana na qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Mahmoud Khalil al Husari ambaye alisoma Qur'ani katika baadhi ya mikitano.

Klipu hii hapa chini ni ya qiraa ya Sheikh al-Husari akiseoma aya katika Sura Ash-Shura katika moja vikao mjini Tehran.

 

 

3967599

captcha