IQNA

Paul Pogba wa Manchester United anafunga Saumu ya Ramadhani wakati wa mechi

19:54 - April 24, 2021
Habari ID: 3473846
TEHRAN (IQNA)- Paul Pogba, mchezaji mahiri wa timu ya Manchester United katika Ligi Kuu ya Premier nchini Uingereza anasema atakuwa amefunga saumu ya Ramadhani wakati wa mechi baina ya timu yake na Leeds United Jumapili 25 Aprili mchana.

Pogba ambaye ni miongoni mwa wachezaji maarufu Waislamu katika Ligi ya Premier amesema mechi hiyo itakuwa ni muhimu sana kwake kwani ni ya 200 tokea aanze kuichezea Manchester United ambayo ni moja ya tibu bora zaidi za klabu duniani.

Akijibu swali kuhusu Saumu ya Ramadhani wakati wa mechi amesema: “Naweza kusema kuwa nimeshazoea. Nimekuwa nikifunga Saumu wakati wa mechi kwa miaka mingi sasa. Nina mtaalamu wa lishe ambaye hunisaidia na kunishauri kuhusu kile ninachopaswa kula.” Ameongeza kuwa: “Nina bahati kuwa hakuna joto sana wakati huu kwa hivyo sihisi ugumu sana.”

Pogba ambaye ni mchezaji wa kiungo cha kati ni miongoni mwa wachezaji ghali zaidi wa soka duniani alijiunga na Machester United mwaka 2016 kutoka Juventus ya Italia ambapo alinunuliwa kwa Euro 105.

Anasema mama yake ni Mwislamu lakini katika familia yake hawakufuata mafundisho ya Kiislamu utotoni. Hatahivyo Pogba anasema baadaye akiwa kijana aliamua kuufuata Uislamu kikamilifu baada ya kuwa na marafiki wenye imani thabiti.

Baada ya kupitia kipindi kigumu katika maisha ya binafsi, Pogba alienda kutekeleza ibada ya Umrah katika mji Mtakatifu wa Makka mwaka huu. Anasema: " Sikuzaliwa Mwislamu ingawa mama yangu alikuwa Mwislamu. Nililelewa kwa msingi wa kuwaheshimu wote." Anaongeza kuwa, alikuwa na marafiki wengi na katika mazungumzo nao alianza kujiuliza maswali mengi sammba na na kufanya utaifiti. "Wakati moja niliswali pamoja na marafiki zangu na nilipata hisia nzuri na iliyo tafauti." Anasema baada ya hapo aliamua kusilimu na akawa anaswali sala tano kwa siku na kutekeleza mafundisho mengine yote ya Kiislamu ikiwa ni pamoja na Saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

3474542

captcha