IQNA

Hamas na Jihad Islami zaunga mkono mwamko wa Wapalestina dhidi ya Wazayuni

13:10 - June 28, 2020
Habari ID: 3472907
TEHRAN (IQNA) – Harakati za mapambano ya kupigania ukombozi wa Palestina za Hamas na Jihad Islami zimetangaza kuunga mkono harakati za wananchi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya njama za utawala wa Kizayuni za kuteka eneo hilo.

Katika taarifa ya pamoja Jumamosi, harakati hizo mbili zimeunga mkono jitihada zote za Wapalestina za kukabiliana na njama hiyo ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Taarifa hiyo ya pamoja imetolewa baada ya mkutano wa Kiongozi wa Hamas Ismail Haniya na kiongozi wa Jihad Islami Ziyad al-Nakhalah.

Utawala haramu wa Israel umepanga kutekeleza mpango wa kutwaa asilimia 30 ya eneo la Palestina la Ukingo wa Magharibi na kuliunganisha na ardhi nyingine zilizoghusubiwa za Palestina ifikapo tarehe Mosi mwezi Julai mwaka huu wa 2020. 

Mpango wa utawala haramu wa Israel wa kutwaa asilimia 30 ya eneo la Palestina la Ukingo wa Magharibi na kuliunganisha na ardhi nyingine zilizoghusubiwa za Palestina ni miongoni mwa vipengee muhimu vya mpango wa kibaguzi wa “Muamala wa Karne”. Benjamin Netanyahu, kiongozi wa chama cha Likud na Benny Gantz kiongozi wa chama cha Blu na Nyeupe, walifikia makubaliano ya kutwaa asilimia 30 ya eneo la Palestina la Ukingo wa Magharibi na kuliunganisha na ardhi nyingine zilizoghusubiwa za Palestina. Mpango huo umepingwa vikali na Wapalestina na jamii ya kimataifa.

3907237

captcha