IQNA

Misikiti yafunguliwa tena Misri lakini kwa masharti makali ya kiafya

22:23 - June 26, 2020
Habari ID: 3472901
TEHRAN (IQNA) - Misikiti kote Misri inafunguliwa tena kuanzia Juni 27 lakini kwa kuzingatia masharti makali ya kiafya ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Kwa mujibu wa tovuti ya Al Ahram serikali ya Misri pia imeondoa sheria ya kutotoka nje usiku ili kupunguza athari mbaya za kiuchumi za janga la COVID-19.
Kwa mujibu wa sheria mpya, misikiti ambayo pamoja na makanisa iliyofunguwa kuanzia Machi, itafunguliwa tena kwa kuzingatia sheria mpya za kiafya. Kati ya sheria hizo ni kwalazimu waumini kuvaa barakoa, kuja misikiti wakiwa na zulia au msala binafsi na kushika wudhuu nyumbani au maeneo mengine lakini si msikitini. Aidha vyoo vya misikiti vitafungwa, ni misikiti mikubwa tu itakayofunguliwa na maeneo ya wanawake hayatafunguliwa. Watoto pia hawataruhusiwa kuingia misikitini.
Halikadhalika waumini wametakiwa wasikaribiane wakati wa swala na alama maalumu zimewekwa ili kuainisha sehemu ya kusimama wakati wa kuswali. Halikadhalika kwa sasa hakuna ruhusa ya swala ya Ijumaa na misikitini inafunguliwa kwa muda wa dakika 30 tu kwa ajili ya swala za jamaa.

Misri imeshuhudia ongezeko kubwa la maambukizi ya COVID-19 ambapo kufikia Alhamisi watu 61,130 walikuwa wamebukizwa huku 2,533 wakifariki dunia.

Misikiti yafunguliwa tena Misri lakini kwa masharti makali ya kiafya

3906948

captcha