IQNA

Idadi kubwa ya watu New Zealand wasilimu baada ya hujuma dhidi ya msikiti

20:34 - August 19, 2019
Habari ID: 3472091
TEHRAN (IQNA) – Mkaazi wa Canterbury, New Zealand anasema alivutiwa na Uislamu na kuamua kusilimu baada ya hujuma dhidi ya misikiti katika mji wa Christchurch nchini humo.

"Daima nilikuwa natafuta sehemu ambayo ningeweza kupata utulivu lakini sikufanikiwa kwa muda mrefu," anasema Bi. Megan Lovelady, 22.

Baada ya gaidi kushambulia misikiti miwili katika mji wa Christchurch mwaka huu, Megan alianza kufanya utafiti wa kina na hatimaye alisilimu. Hivi sasa Megan huswali mara kwa mara katika Msikiti wa Al Noor, ambao ni kati ya misikiti miwili iliyoshambuliwa mjini Christchurch.

Bi. Megan anasema kabla ya mashambulizi hayo, alikuwa amechanganyikiwa kuhusu maisha na hakuwa na uhakika kuhusu muelekeo wake.

Bi. Megan ambaye anafanya kazi katika seta ya utalii alihamia Christchurch New Zealand pamoja na familia yake akiwa na umri wa miaka saba.

Anasema alipata msiba mkubwa maishani wakati mchumba wake alipoagad dunia baada ya kugongwa na treni na hivyo maisha yake yalikumbwa na msukosuko mkubwa wa kimaanawi. Hali hiyo ya kukosa mueleko wa kidini maishani iliendelea hadi matukio ya kushambuliwa misikiti miwili mjini Christchurch mnamo Machi 15, 2019 na hapo maisha yake yalishuhudia mabaduliko makubwa.

Katika Ijumaa ya kwanza baada ya mashambulio hayo ya kigaidi alikuwa miongoni mwa maelefu ya raia wa New Zealand wasio Waislamu waliojiunga na Waislamu katika Sala ya Ijumaa ili kuonyesha mshikamano na Waislamu. Anasema aliposhiriki katika Sala ya Ijumaa kama mtazamaji katika Bustani ya Hagley, alivutiwa sana na hotuba ya Imamu wa msikiti na namna Waislamu walivyokuwa wakiswali kwa nidhamu. Mandahri hiyo ya kuvutia ya Sala ya Ijumaa iliibua hisia ya kipekee ya kimaanawi  na utulivu na hapo akatokwa na machozi.

Baada ya kutafakari kuhusu hisia hiyo, Bi.Megan anasema alihisi ni kana kwamba daima alikuwa Mwislamu. Bi. Megan aliamua kuukumbatia Uislamu maishani na baada ya kusilimu amekuwa akifika msikitini kila siku kuswali na kujifunza kusoma Qur'ani na kupata mafunzo jumla ya Uislamu.

Kwa mujibu wa Imam Nizamul Haq Thanvi, wa Jumuiya ya Kimataifa ya Waislamu New Zealand, punde baada ya misikiti kushambuliwa mjini Christchurch na Waislamu 51 kuuawa wakati wa Sala ya Ijumaa, kwa wastani baina ya watu watatu na watano wamekuwa wakisilimu katika msikiti mmoja mjini Wellington na hali hiyo pia imeripotiwa katika maeneo mbali mbali nchini New Zealand.

3469200

captcha