IQNA

Treni ya Kasi kutoa huduma kwa Mahujaji mwaka huu

18:53 - August 09, 2019
Habari ID: 3472076
TEHRAN (IQNA) - Huduma ya treni ya mwendo kasi itaanza kutumika kwa mara ya kwanza mwaka huu katika Ibada ya Hija.

Baadhi ya Waislamu zaidi ya milioni mbili na nusu wanaoshiriki katika Ibada ya Hija mwaka huu wanatazamiwa kutumia treni hiyo inayojulikana kama Haramain High Speed Rail (HHR), ambayo inaunganihsa Makka na Madina na pia inaungaanisha Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Mfalme Abdul Aziz mjini Jeddah na Mji wa Kiuchumi wa Mfalme Abdullah huko Rabigh.
Treni hiyo Oktonba 2018 na hivyo mwaka huu itakuwa mara ya kwanza kutumiwa na Mahujaji. Safari ya barabarani baina ya Makka na Madina kwa kawaida huchukua hadi masaa 10 wakati wa msimu wa Hija lakini sasa safari hiyo itachukua takribani masaa mawili kwa wale wanaotumia treni ya HHR.
Treni hiyo inaweza kusafiri kwa mwendo wa hadi kilomita 300 kwa saa katika reli ya umeme. Kwa ujumla HHR ina treni 35, na kila treni ina mabehewa 13 yenye viti 417 katika daraja za kwanza na pili. Aidha HHR ina uwezo wa kubebe abiria milioni 60 kwa mwaka.

3469133

captcha