IQNA

Jeshi la Iran kuanzisha vituo 50 vya kuhifadhi Qur'ani

23:38 - July 11, 2019
Habari ID: 3472039
TEHRAN (IQNA) - Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lina mpango wa kuanzisha vituo 50 vya kuhifadhi Qur'ani (Darul Tahfidhul Qur'an) katika vitengo kadhaa vya jeshi hilo.

Hayo yamedokezwa na mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Umma katika Jeshi la Iran, Hujjatul Islam Sayyed Akbar Mousavi wakati wa sherehe za kufungwa Mashindano ya Qur'ani ya Askari wa Jeshi la Nchi Kavi la Iran  mjini Isfahan kati mwa Iran wiki hii.
Ameongeza kuwa tayari vituo 38 vya kuhifadhi Qur'ani vinakaribia kufunguliwa.
Sheikh Akbar Mousavi ameongeza kuwa, leo kuneshuhudiwa ongezeko kubwa la harakati za Qur'ani katika Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na majeshi mengine ya Iran.
Amesisitiza kuwa, utamaduni wa Qur'ani ndio nguzo kuu katika uwezo wa kujihami wa majeshi ya Iran.
Mashindano hayo ya Qur'ani yaliwashirikisha maafisa 300 wa Jeshi la Iran pamoja na familia zao.

3468927

Kishikizo: iran jeshi iqna
captcha