IQNA

Mkutano wa Changamoto za Umma wa Kiislamu wafanyika Uturuki

19:59 - October 15, 2018
Habari ID: 3471709
TEHRAN (IQNA)- Wasomi kutoka nchi mbali mbali wamekutananchini Uturuki kujadili changamoto za ulimwengu wa Kiislamu chini ya anuani ya 'Kongamano la Kimataifa la Ummah wa Kiislamu."

Kongamano hilo ambalo lilianza Jumapili na kuendelea kwa siku tatu liliwaleta pamoja wanazuoni maarufu 20 za Kiislamu na liliandaliwa na Kituo cha Uislamu na Masuala ya Kimataifa katika Chuo Kiku Cha Sabahattin Zaima mjini Istanbul.
Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano hilo, Sami al Arian ambay ni mkurugenzi wa kituo hicho amesema kongamano hilo limejadili matatizo yote yanayowakumba Waislamu duniani.
Amesema mada kuu nne za kongamano hilo ni matatizo ambayo Waislamu wanakabiliana nayo duniani ambayo ni malumbano ya kimadhehebu, usekulari, utaifa na ubeberu.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sabahattin Zaima , Mehmet Bulut amesema masuala hayo manne yanaendelea kuwa shinikizo kubwa kwa Waislamu na hivyo kuathiri maisha na hatima yao kote duniani.

3466985

captcha